
Msanii wa muziki wa Bongoflava ambaye anaiwakilisha vizuri Tanzania nje ya mipaka ya nchi, Sa Raha amepata shavu la kuingia katika mashindano ya muziki ya kimataifa yanayofahamika kama Global Rockstar - Music Contest 2013, ambayo yanapambanisha zaidi ya wasanii 73 kutoka nchi 73 tofauti duniani.
Saraha ameingia katika shindano hili kupitia wimbo wake wa Jambazi, na mpaka sasa amefanikiwa kufikia hatua ya 16 bora, ambapo Novemba 16 kutafanyika onyesho kubwa kabisa la kazi za washiriki huko Vienna na mwisho wa siku mshindi wa shindano hili atajipatia zawadi ya dola 10,000 za Marekani.
Kupitia mahojiano yake na eNewz, Saraha amewaomba watanzania kumpigia kura na kumwezesha kushinda mashindano haya kupitia mtandao wa www.global-rockstar.com, ambapo pia itakuwa ni nafasi ya kipekee ya kutangaza zaidi muziki wa Bongoflava duniani.
No comments:
Post a Comment