DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Tuesday, November 26, 2013

Mtoto wa Ice Prince Jukwaani

 
Ice Prince ameonyesha ni kwa jinsi gani anajivunia kuwa baba, kwa kumpandisha mtoto wake anayefahamika kwa jina Jamal na kumuonyesha kwa umati mkubwa wa mashabiki waliokuwa wamehudhuria onyesho lake la uzinduzi wa albam Fire of Zamani.

Msanii huyu amefanya kitendo hiki cha kipekee wakati alipokuwa akiimba Live wimbo wake maarufu wa Aboki, ambapo alimuonyesha mwanae kwa mashabiki jukwaani, kitendo kilichotafsirika kama njia mojawapo ya kuanza kumfundisha dogo kazi ya kupiga shoo.

Uzinduzi wa albam ya msanii huyu huko Nigeria umekuwa ni wa mafanikio makubwa na hatua nyingine ya kimaendeleo kwenye sanaa ya staa huyu ambaye anashikilia tuzo ya BET ya msanii bora wa kimataifa kutoka Afrika.

No comments: