DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Tuesday, November 19, 2013

MWANA FA : KUONDOKA EAST COAST KUMENILETEA MAFANIKIO MAKUBWA



Akiwa kwenye matembezi barani Amereka, Mwana FA alipata nafasi ya kufanya mahojiano na Vijimambo Tv na kufunguka maswala mengi kuhusiana na lina msanii huyo atafunga ndoa pamoja na swala zima la East Coast.

Alipoulizwa swali kwamba ni muda mwingi umepita na hatujui East Coast iko wapi? Mwana FA alijibu swali hilo kwa kuzingatia sana swala zima la kibiashara pamoja na soko la muziki wake. Mwana FA alisema ” Yeye na AY ndio walijitoa kwenye East Coast ili kupunguza migogoro au beef na wasanii wengine, pia wasiathirike kibiashara, pamoja na kuufanya muziki wao uwapatie riziki.”
Aliendelea kwa kusema “Baada ya yeye kujitoa East Coast ndicho kipindi alipata sana mafanikio ya muziki wake”.

No comments: