DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Tuesday, November 19, 2013

Msomi Nikki aeleza Mipango


 
Kwa mara ya kwanza kabisa baada ya kufanikiwa kumaliza masomo yake ya Shahada ya Uzamili, katika fani ya Maendeleo ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rapa Nikki wa Pili ameongea na eNewz kuhusiana na mpango wake wa maisha ya sanaa na ya kitaaluma.

Rapa huyu ambaye ameonyesha uwezo wa ajabu wa kuweza kufanya muziki katika kiwango cha hali ya juu na pia kuweza kuendelea na masomo mpaka ngazi hii ya juu, amesema kuwa malengo pamoja na kuwa na mpango ni moja kati ya mambo ambayo yamechangia katika mafanikio ambayo ameyapata mpaka sasa.

Nikki amesema kuwa, kwa sasa baada ya kumaliza masomo, amefikiria kuanzisha shughuli kadhaa ambazo anaziona kuwa zinaweza kumsaidia kuendesha maisha, ambapo amesema kuwa kwa nafasi ndogo sana anafikiria kupata ajira ama kuajiriwa, na muziki utaendelea kuwa ni kama mke wake ambaye hawatatengana mpaka mwisho wa maisha yake.

No comments: