
Ney ambaye anasisitiza kuwa kiuhalisia yeye ni rapa, ameweka wazi kuwa nyimbo yake ya kwanza kuimba ambayo inafahamika kwa jina 'Hellow' ndiyo iliyopandisha dau la kiwango cha pesa alichokuwa analipwa kwa shoo hapo awali na kumfanya aamini kuwa anaweza kuendesha maisha yake kupitia muziki.
Ney amesema kuwa, anafurahi kuwa katika muziki wake kuna kundi kubwa sana la watu ambao wanamkubali vilivyo pale anaporap, na vilevile kundi lingine kubwa zaidi linamkubwali sana anapofanya miondoko ya rap, na hawa ndio wakali wanaomfanya anaendesha maisha yake ama anafanya biashara kupitia muziki.
No comments:
Post a Comment