DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, November 13, 2013

NIKKI MBISHI: SIJUI FAIDA YA ‘SAUTI YA JOGOO’

























Nicas John Marwa a.k.a Nikki Mbishi ni miongoni mwa kizazi cha sasa cha Hip Hop kinachotingisha zaidi kwenye kiwanda cha mziki wetu hapa Bongo.
Tarehe 26 November 2011, Nikki mbishi aliingiza sokoni album yenye ngoma nyingi kali kama vile Play Boy, Nyakati, Au n.k ambayo ilikuwa inajulikana kwa jina la ‘Sauti ya Jogoo’.

Albamu hiyo ilitoka chini ya record lebo ya M-Lab kipindi hicho akiwa yupo chini ya Lebo hiyo ambayo baadae aliihama na kuingia Tamaduni Muzik ambayo yupo hadi sasa akiwa kama General Manager. Akizungumzia mauzo ya albamu hiyo, Zohan a.k.a Baba Malcom amesema hajawahi kupokea chochote kama mauzo ya albamu hiyo.
“kiukweli sikupata hata senti tano kupitia album hiyo kwani kipindi kicho nilikuwa shule na hata nilivyorudi hawakunijuza chochote naamini iliuza sana kwani hadi Hashim Thabit alinunua album hiyo kwa hiyo sikutaka kuwaauliza kwani hivyo ni vitu vidogo ambavyo haviwezi kutukosesha kuaminiana kwa hiyo nikaachana nayo” – Nikki Mbishi.r.

No comments: