Ikiwa imebaki siku moja tu kabla ya show ya kihistoria inayosubiriwa na
wengi kufanyika ndani ya viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam,
tayari jukwaa litakalotumiwa na wasanii wanne kutoka hapa nyumbani na
wale wakali wa kulishambulia jukwaa barani Afrika P~Square lipo katika
maandalizi ya mwisho mwisho pamoja na kufunga mziki.
Jukwaa lina sehemu tatu za kupandia juu yaani ngazi na vijukwaa
vidogo viwili kama winchi vilivyopo katikati ya stage. Imefungwa sound
yenye mjumuiko wa spika zaidi ya sitini ambapo ufungaji wa sound
unaendelea sambamba na kufunga stage ambayo inaweza kukamilika siku ya
kesho.
Kumbuka kuwa wasanii watakao-perform jukwaa moja na P` Square ni
Malkia wa Bongo fleva mwenye miaka kumi na tatu kwenye gemu Lady Jay Dee
a.k.a Anaconda, King wa R&B Ben Paul, mwamba wa kaskazini Joh
Makini na MC shupavu au Heavy weight Mc au Daddy Joseph Haule wa
Mitulinga Mchawi wa Rhymes. Hii si ya kukosa kwasababu kwa mara ya
kwanza utashuhudia show nzima ikidondoshwa kwa style ya kupiga live
band.
Na hizi ni baadhi ya picha zikionesha jukwaa hilo likiwa liknaendelea kutengenezwa
Na hizi ni baadhi ya picha zikionesha jukwaa hilo likiwa liknaendelea kutengenezwa



No comments:
Post a Comment