
Siku ya jana tarehe 23/11/2013 katika viwanja vya Leaders Club ilikuwa
ni siku ya ma-legendary wa East na West Africa wenye uwezo wa kuimba
live na kutumia stage kwa namna yake.
Baada ya wasanii wa Kibongo kama vile Ben Pol, Lady Jaydee, Prof. Jay
na Joh Makini kupanda juu ya Jukwaa na kuanza kuwapagawisha mashabiki
kwa aina tofauti tofauti kwa masong yao kibao yanayotamba kwa Redio na
Tv stations.
Muda ukawadia kwa wakali wa stage Africa P-Square kuingia Jukwaani na
kuanza kufanya show non stop kwa ngoma zao za zamani na mpya kwa
takribani masaa mawili na madakika kibao.
Paul na Peter walidhihilisha wazi kwa mashabiki wa Tzee kuwa wana
uwezo wa kutumia Jukwaa, hakika kila mtu aliyeondoka pale alikuwa
anawazungumzia PSquare kwa show yao bomba, Pia ilikuwa kama fundisho kwa
wasanii wa kibongo wanaofanya show kwa desturi.

No comments:
Post a Comment