DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, November 1, 2013

Stara ahamasisha wasichana


 
Msanii Stara Thomas ameendelea kutumia nafasi na kipaji chake kuangazia jamii ya Tanzania juu ya tatizo la Mimba za Utotoni akihirikiana na Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia ongezeko la Watu Duniani (UNFPA).

Stara kupitia nafasi hii, pia ameweza ya kutumbuiza wimbo wa kuhamasisha uzazi wa mpango katika familia katika tukio kubwa la uzinduzi wa ripoti ya mwaka 2013 ya hali ya idadi ya watu duniani ambayo hutayarishwa na UNFPA, lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Tukio hili ni moja ya mchango mkubwa wa mwanamama Stara Kusaidia harakati za mfuko huu wa umoja wa kimataifa katika kupambana na tatizo la mimba za utotoni kwa wasichana hapa Tanzania.

No comments: