
Wasanii kutoka hapa Bongo ambao wamechukua shavu la kupiga show Live Jukwaa moja na P Square siku ya Jumamosi tarehe 23 Novemba 2013 jijini Dar es Salaam wametangazwa rasmi leo tayari kabisa kwa kukinukisha katika show hii kihistoria.
Wasanii hao ni Ben Pol, Professa Jay, Lady Jay Dee pamoja na Joh Makini ambao watatikisa juu ya jukwaa lenye Uzito katika kiwanja cha Leaders Club ambapo muziki utakuwa si wa kitoto.
Wakali hawa tayari wameingia katika kujipanga kudondosha show la aina yake hasa ikizingatiwa kuwa hii ni kama dhamana ya kuwakilisha vipaji vilivyoko hapa Bongo, dhidi ya wasanii hawa ambao wamekuwa ni kivutia katika anga la kimataifa.
Zoezi la kununua tiketi linaendelea kwa njia ya Vodacom M-Pesa kwa shilingi 30000 tu za kitanzania mpaka tarehe 17, ambapo kwa siku zinazobakia ticketi zitauzwa kwa shilingi 35000 madukani.
Kumbuka, Ni P Square Live in Dar, Hii si ya kukosa.
No comments:
Post a Comment