
Mara baada ya kumaliza tofauti yake na aliyekuwa prodyuza wake Man Water, wameingia tena chumba cha sindano na kugonga kopo kadhaa ikiwemo ‘Subira Yavuta Heri’ ambayo ndiyo itakayoanza kuachiwa kwenye project ambayo wanafanya na Man Water ndani ya Combination Sound.
“Yap! Mara zote kazi zangu zinalenga zaidi kufundisha na kuelimisha jamii huku kuburudisha kukichukua sehemu ndogo sana ndio maana huwezi ukaifananisha ngoma yangu na mtu mwingine.” – 20 Percent.
“Kikubwa ni kwamba kama unavyojua nilimpoteza baba yamgu mzazi so nasubiri kwanza tufanye arobaini yam zee, halafu tuanze kuachia ngoma moja baada ya nyingine zikitokea palepale kwa Man Maji Combinenga, Much love kwa fans wote, 20 nakuja tena kuubariki huu mziki.” – 20Percent.
20% aliwahi kuuteka huu mziki wa Bongo na ngoma kali kama vile Tamaa Mbaya, Mama Neema, Naficha, Money Money, Ya nini malumbano n.k. huku akiwa ni msanii wa kwanza wa Bongo Fleva kutumia nyimbo zake na kuibuka na filamu kali iliyoteka hisia za wengi iliyokwenda kwa jina la ‘Furaha Ipo Wapi’.
KARIBU TENA BROTHER…!!!
No comments:
Post a Comment