
Akiongea na ENewz ya EATV, Belle ametanabaisha kuwa isingekuwa rahisi kwake kueleweka kwa fans wake kwasababu amekaa muda mrefu sana bila kutoa wimbo tangu pale alipoachia ‘Listen’ mwanzoni mwa mwaka huu kisha aibuke hapa mwishoni na kusema anaachia album.
“Album iko palepale lakini kitu kilichofanya tusiitoe sasa hivi ni kwamba tulisitisha mimi na uongozi wangu baada ya kuona nipo kimya sana halafu ule ukimya uje utangaze tu natoa album, nisingeeleweka that’s why nimetoa kwanza hii wanitamani ili watu wajue niko around pia naendelea kufanya kama kawaida lakini album itakuja.” – Belle 9
“Hata kama angekuwa nani, huwezi kukaa kimya mwaka mzima halafu ukatangaza album ijapokuwa Beyonce kafanya hivyo lakini mimi niliona hapana itakuwa sio poa.” – Belle 9.
No comments:
Post a Comment