Shindano hilo la EBSS 2013, lilikuwa limebakiza washiriki watano tu amabao walifanikiwa kuingia katika fainali za kumsaka star mpya wa shindano hilo, washiriki hao walikuwa ni Amina Chibaba, Emmanuel Msuya, Elizabeth Mwakijambile, Maina Thadei na Melissa John.

Emmanuel Msuya alifanikiwa kuwabwaka washiriki wenzake wanne katika shindano hilo na kufanikiwa kunyakua kitita cha sh milioni 50, pamoja na mkataba mnono wa kurekodi katika moja ya studio kubwa hapa nchini za MJ Records.
No comments:
Post a Comment