DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, January 8, 2014

Bastola za Jude zazua mjadala

 

Kaka wa P Square, Jude Okoye amezusha mjadala mkubwa katika mitandao ya jamii hasa baada ya kuweka picha inayomuonyesha akiwa na bastola pamoja na risasi zake, ikiwa ni moja ya hatua za kuwaonyesha kuwa amejikamilisha kwa upande wa ulinzi.

Baada ya Jude kuweka picha hii, asilimia kubwa ya mashabiki waliotoa maoni wamesema kuwa haikuwa busara kwa Jude kuonyesha jamii picha ya namna hii kutokana na asilimia kubwa ya vijana kupenda kuwaiga mastaa hawa hususan P Square, na kufanya kila wanachokuwa wanafikanya.

Kutokana na mtazamo huu, picha ya Jude imeonekana kama moja ya vishawishi  kwa vijana kumiliki silaha za moto, kitu ambacho ni hatari sana kwa jamii, ingawa kwa upande mwingine kumekuwa na mashabiki ambao wameunga mkono kwa asilimia zote hatua ya Jude kuonyesha bastola.

No comments: