DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, January 8, 2014

Witnesz; Sichagui show

 

Msanii wa muziki Witnesz, ambaye ni moja ya marapa ambao bado wana nguvu kubwa hapa Bongo, amesema kuwa amejipanga vilivyo kwa ajili ya kufanya biashara ya muziki kwa mwaka huu, ambapo hatakuwa anachagua sehemu ya kufanya shoo endapo atapatiwa dili na kufikia maelewano mazuri na kati yake na mratibu ama waratibu wa shoo husika.

Kwa upande wa kazi zake, Msanii huyu pia ameweka wazi kuwa kwa sasa ana ngoma mbili ambazo zipo tayari kabisa, audio pamoja na Video na mpaka mwishoni mwa wiki hii atakuwa amekwishaachia moja kati ya hizo.

Msanii huyu amesema kuwa, safari hii atatoka yeye pamoja na mdogo wake anayejulikana kwa jina CBH pamoja na Ochu Sheggy ambaye wamekwishatamba naye sana na ngoma inayokwenda kwa jina zaga zaga.

No comments: