DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, January 3, 2014

Chameleone, Goodlyf jukwaa moja

 

 Wasanii Jose Chameleone pamoja na kundi la Goodlyf wameandika historia mpya katika tasnia ya burudani nchini Uganda baada ya kuukaribisha mwaka mpya kwa onyesho la pamoja na katika jukwaa moja katika ukumbi wa hoteli moja maarufu iliyopo ndani ya jiji la Kampala.

Onyesho hili la pamoja la mastaa hawa ambao walikuwa ni mahasimu wakubwa limekuwa ni moja kati ya ishara muhimu ya mwanzo mpya wa mahusiano ya amani kati ya Goodlyf na Chameleone kutoka lebo ya Leone Island.

Chanzo cha ugomvi mkubwa uliokuwepo kati ya pande hizi mbili ni kujitoa kwa Goodlyf chini ya lebo ya Leone Island ambayo inasimamiwa na Chameleone mwaka 2008, na kufanya kazi zao kwa kujitegemea huku Chameleone akitafsiri hatua hii kama kuvunjiwa heshima baada ya kuwasaidia sana kimuziki.

No comments: