Mastaa wa muziki Bongo, wamekuwa na mtazamo wa tofauti kufuatia taarifa
za kukamatwa kwa mrembo Jackie Cliff kwa tuhuma za kusafirisha Dawa za
kulevya huko China, kati yao akiwepo Dyna ambaye ametoa maelezo marefu
kuwataka watu kutokukimbilia kutoa hukumu ya moja kwa moja kwa mrembo
huyu pasipo kujua uhalisia wa tukio lenyewe kwa undani.
Kwa upande mwingine, Ray C ambaye ndiyo kwanza ametoka katika shimo la uathirikwa wa dawa hizi za kulevya, ametaka sheria kuchukua mkondo wake bila huruma kwa mrembo huyu mtanzania aliyekamatwa, mtazamo ambao umepokelewa tofauti na asilimia kubwa ya watu.
Mpaka sasa bado hakuna taarifa za ndani juu ya mustakabadhi wa mrembo huyu kutoka Tanzania ambaye yupo chini ya Ulinzi huko China kwa kosa hili kubwa ambalo hukumu yake nchini humo huwa ni kunyongwa mpaka kufa.

No comments:
Post a Comment