Mo Racka & AY
Kwa wale
wapenzi wa kazi za rapper Mo Racka, msanii huyu baada ya kimya cha
karibia mwaka mzima wa 2013… rapper huyu ameamua kuuanza mwaka mpya na
ngoma mpya ambayo anatarajia kuiachia rasmi tarehe 6 mwezi huu wa kwanza
siku ya Jumatatu.
Mo Racka amesema ngoma
yake hiyo mpya ameipia tittle ya USISOGEE, ikiwa ni kazi iliyofanyikia
katika studio yake iitwayo My Record, jijini Dar-Es-Salaam.
Pia katika ngoma hiyo msanii huyu mahiri amesema utapata kusikia sauti
za wasanii wengine wawili ambao amewashirikisha katika wimbo huo mpya.
No comments:
Post a Comment