Msanii aliyoko juu na mwenye fedha nyingi nchini Kenya, hit make wa KIGEUGEU na KIPEPEO msanii Charles Njagua Kanyi AKA Jaguar yupo katika maandalizi ya kufyatua video
mpya ya wimbo wake uitwao KIOO, ambapo wimbo huu ameufanhyia katika
magereza ya viwanda/Industrial Prison nchini Kenya katika jiji la
Nairobi.
Jaguar akiwa amevalia gwanda za wafungwa
Hivi karibuni msanii huyu
iliripotiwa kuwa alitumia baadhi ya muda wake wa siku kuu mwaka jana
kukaa, kuwasaidia na kusherekea na wafungwa katika magereza ya
viwanda/Industrial Prison jijini Nairobi Kenya. Msanii
huyu mwenye roho nzuri ya kusaidia Jamii, anatarajia kuachia video ya
wimbo wake huo mpya wa KIOO siku ya jumatatu mwezi huu.
No comments:
Post a Comment