Msanii mkongwe wa Hip Hop
na kiongozi wa kundi la Hip Hop lijulikanalo kwa jina la Kikosi cha
Mizinga… Kala Pina, ameandaa project nyingine ya Tanzania Bila Dawa
itakayo anza rasmi mwezi wa tatu mwaka huu 2014 baada ya project ya Hip
Hop Bila Madawa kuleta mafanikio. Msanii huyu amesema kuwa project hii
ya sasa inalenga kuelezea kilio cha wasanii katika kupiga vita biashara
haramu ya madawa yakulevya ambayo tayari imeshaenea katika maisha ya
baadhi ya wasanii na inazidi kuangamiza maisha ya vijana ambao ndio
nguvu kazi ya taifa katika maendelo ya nchi yetu.
Hip Hop Bila Madawa
Ilikuwa project ambayo inalenga wasanii na vijana walioko katika
harakati za Hip Hop, na sasa Kala Pina ameamua kuleta project pana zaidi
ambayo itajumuisha wasanii wote na Taifa letu kiujumla, na ndomana
project hii mpya itaitwa Tanzania
Bila Dawa. Project hii itakayo zinduliwa rasmi mwezi March mwaka huu wa
2014 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es saalam na baadae kusambaa
kwenye miji mengine kama Mwanza, Arusha na mikoa mingine pia ina lengo
la kuchangisha fedha ili kuweza kuwasaidia vijana wengineo ambao tayari
wamesha athirika na matumizi ya madawa ya kulevya hapa nchini.
No comments:
Post a Comment