Wahu, Staa wa muziki na mama wa watoto wawili kutoka huko nchini Kenya,
ameweka wazi kuwa kwa sasa anaingia katika ratiba kali ya mazoezi kwa
ajili ya kuurudisha mwili wake katika shape nzuri wakati huu ambao mtoto
wake anakaribia kufikia umri wa miezi 6.
Wahu amesema kuwa, anaona huu ndio wakati muafaka wa kufanya hivyo hasa kutokana na kushuhudia wanawake wengi wakijisahau na kujiachia pale wanapoongezeka uzito baada ya kujifungua, na hivyo kusababisha kupoteza mvuto na muonekano mzuri.
Wahu amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuwapatia mashabiki wake taarifa mbalimbali za muhimu kuhusiana na wakina mama na malezi ya watoto kwa njia ya mtandao, kazi ambayo siku hadi siku imekuwa na mchango mkubwa katika kuelimisha watu mambo muhumu juu ya malezi.

No comments:
Post a Comment