DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, January 31, 2014

Wengi wamzika Mama Gentriez

 

 Wasanii wa muziki kutoka Jijini Arusha, leo hii wameonyesha umoja na sapoti ya kutosha kwa msanii mwenzao Gentriez Mwakitabu katika maziko ya mama yake mzazi aliyefariki juzi kwa ugonjwa wa moyo.

Miongoni mwa umati mkubwa uliohudhuria msiba huu huko Sinoni Daraja Mbili Arusha, ni pamoja na rapa Joh Makini, Kundi la muziki la Jambo Squad, Mtayarishaji muziki mahiri John B kutoka Grandmasters na wengine wengi.

DJ-BOSTON BLOG inamtakia msanii huyu faraja na utulivu katika kipindi hiki kigumu anachopitia na Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya mama Gentriez. Aamin.

No comments: