Rapa M Rap, baada ya kutoka kwa misukosuko chini ya lebo ya B Hitz hivi
karibuni, ametangaza ujio wake mpya kutoka AM Records, kwa kuja na traki
yake mpya inayokwenda kwa jina “Usiende Mbali” ambayo ndani yake
amemshirikisha na msanii Jux Vuitton.
M
Rap amesema kuwa kazi hii mpya inabeba ujumbe wa mapenzi kwa ajili ya
kuwapa moyo wapendanao ili kudumisha zaidi mahusiano yao, na kusema kuwa
kazi hii mpya ndio mwanzo wa kufungua vyema mwaka huu wa 2014.
Aidha rapa huyu amewaomba mashabiki na wadau wote kuumpa sapoti kwani
kazi zingine mpya zinatarajiwa kukamilika katikati ya mwaka huu.
No comments:
Post a Comment