Staa wa muziki wa Bongoflava, Ommy Dimpoz amewaahidi mashabiki wake
kuachia kazi mpya ambayo itakuwa gumzo la Jiji hivi karibuni ikiambatana
na video ambayo amewekeza pesa nyingi kuifanya huko nchini Uingereza,
kazi ambayo itakuwa tayari mwezi huu.
Kuhusiana
na kazi hii mpya ambayo picha zake zimekwisha onekana mitandaoni,
Dimpoz ameweka wazi kuwa imekuwa ni somo kubwa kwake kufanya kazi hii
iliyo katika kiwango cha kimataifa, akiwa chini ya uongozaji wa
mtayarishaji video mkubwa kabisa, Moe Musa ambaye anafanya kazi zake
huko Uingereza.
Ommy Dimpoz amesema kuwa, kutokana na kiasi cha pesa ambacho
amewekeza katika video hii, muda na kufuatilia mpangilio wa ratiba ya
kazi bila kuweka utani, kazi hii itaacha gumzo hapa Tanzania na Afrika
kwa ujumla pindi itakapotoka.
No comments:
Post a Comment