DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, April 17, 2014

MSAANI WA AFRIKA KUSINI ‘OSKIDO’ KUSIKIKA TIMES FM

image
 
Kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm kinaendelea na msimu wa Experience Africa kwa kuwashusha wasanii wa Afrika mwezi huu ambao wanachagua nyimbo tano wanazozipenda zaidi na kujibu maswali. Baada ya kumsikia Orezi wa Nigeria na R2bees wa Ghana Jumapili
zilizopita, Jumapili hii kipindi hicho kitamshusha gwiji wa muziki kutoka Afrika Kusini ‘Oskido’.
Oskido amejipatia umaarufu kwa kazi zake za utayarishaji wa muziki, uandishi na uimbaji. Y-tjukutja ni moja kati ya nyimbo maarufu hivi sasa zilizoandaliwa na Oskido.
“Niliwaahidi wasikilizaji kuwa mwezi huu tutajikita katika kufanya mahojiano na kusikia nyimbo wanazozipenda wasanii wakubwa wa
Afrika waliopo nje ya Tanzania. Unajua tumeshafanya na wasanii wa Tanzania ambao pia ni wakubwa kwa Afrika, lakini tumeona tuupe umaalum mwezi huu wa nne tupate ladha ya wasanii wengine wa nje ambao wanahit Afrika na hata huko duniani,” amesema Omary Tambwe aka Lil Ommy, mtangazaji wa The Playlist.
Kipindi cha The Playlist kinakuwa hewani kupitia 100.5 Times FM kila Jumapili kuanzia saa kumi kamili hadi kumi na moja kamili jioni.

No comments: