DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, April 17, 2014

Msanii Kizito adaiwa kukiri kuhusika katika Ugaidi

 
Msanii wa muziki Kizito Mihigo kutoka nchini Rwanda amedaiwa kukiri kuhusika katika matukio ya kigaidi yaliyokuwa na lengo la kuiangusha serikali ya nchi hiyo, na hii ikiwa ni siku kadhaa tangu alipokamatwa na kuwekwa kizuizina kwa mashtaka haya.
 
 
Mihigo pamoja na wenzake wawili wanatuhumiwa kushirikiana na waasi wengine wa kabila la Kihutu kutoka huko Afrika Kusini na Dr Kongo katika njama za kupanga mashambulizi kwa ajili ya kuiangusha serikali.
Hata hivyo ripoti nyingine zinamtaja Mihigo kama mtu ambaye alikuwa karibu zaidi na chama tawala cha Rwandan Patriotic Front (RPF), na kukamatwa kwake kumekuwa jambo ambalo linashtusha wengi.

No comments: