Msanii wa muziki, Nameless kutoka nchini Kenya, ametolea ufafanuzi jina
la albam yake mpya Before I Retire (B4IR), kuwa haimaanishi kuwa yupo
katika mpango wa kustaafu muziki kama wengi ambavyo wanatafsiri.
Nameless
amesema kuwa, jina la albam hii limetokana na ukimya wake wa muda mrefu
ambao umepelekea wengi kufikiri kuwa amekwishastaafu na kuachana na
muziki, na hapo ndipo alipoamua kurejea na kazi yenye jina kama hili
kuonyesha kuwa anaendelea na ataendelea kufanya muziki zaidi kabla ya
kustaafu.
Nameless amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, kuna vitu vingi zaidi ambavyo anatarajia kufanya katika muziki kabla ya kufikia hatua ya kustaafu.
Nameless amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, kuna vitu vingi zaidi ambavyo anatarajia kufanya katika muziki kabla ya kufikia hatua ya kustaafu.
No comments:
Post a Comment