Msanii wa Hip Hop, Nay Wa Mitego
amepata deal la matangazo na kampuni ya simu itakayomlipa zaidi ya shilingi milioni 70.
amepata deal la matangazo na kampuni ya simu itakayomlipa zaidi ya shilingi milioni 70.
Nay wa Mitego ameiambia BK kuwa mkataba aliosaini utakuwa wazi mwezi ujao.
“Nimeingia mkataba na kampuni ya simu sio kama balozi ni mtu ambaye atakuwa anatumika katika matangazo yao na vitu vingine kwa kipindi cha mwaka mzima,” amesema. “So nafikiri watu wasubirie tarehe moja nitaanza kazi rasmi ndipo nitakuwa huru kuzungumzia mkataba wangu. Mkataba wangu ulikuwa na vikao vingi huku na kule ili kutafuta maslahi, ila namshukuru tumefika makubaliano mazuri nimesaini mkataba wa mwaka mmoja. Naweza sema utanipa pesa nyingi sana huu mkataba, kwasababu utabadilisha baadhi ya viwango vyangu vya show,hata ubora wa kazi zangu, kwahiyo kwangu naweza sema ni hatua muhimu sana. Siwezi leo kuzungumzia kiasi ambacho nitapata ila tambua ni mkataba mzuri sana,ni zaidi ya shilingi milioni 70. Nadhani nitaitamka rasmi baada ya kuanza kazi tarehe moja ninaweza kuzungumza mambo mengi kuhusu mkataba wangu.”
No comments:
Post a Comment