DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Sunday, April 20, 2014

Peter Miles, Desire Luzinda kunani?

 
 

Wasanii wa muziki wa nchini Uganda, Peter Miles pamoja na Desire Luzinda wameanzisha ukaribu unaozua hisia za kuanza kwa mahusiano ya kimapenzi kati yao, hasa baada ya urafiki wao kushika kasi ndani ya siku moja tu walipokutana huko Entebbe.
 
Peter Miles pamoja na Desire ambao hapo awali hawakuwa na urafiki kama huu ulioanza sasa, ndani ya kipindi kifupi tu, wameonesha kuelewana sana ingawa bado hakuna taarifa za uthibitisho kutoka kwa pande zote kama ukaribu huu unamaanisha kitu chochote cha ziada pembeni ya urafiki.
Kwa upande wa Peter Miles, historia inaweka wazi umahiri wa staa huyu katika kutoka na mastaa wenzake ambapo msanii huyu alikwishawahi kuwa na mahusiano na Juliana Kanyomozi na Cleopatra Koheirwe, kitu kinachoaminisha wengi kuwa huenda ukaribu wake na Desire ukawa umefungua ukurasa mwingine wa mapenzi kwa upande wake.
 
 

No comments: