DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, April 9, 2014

WAKAZI AWAFUNGUKIA WAANDAJI WA SHOW YA MAFIKIZOLO

 
WAKAZI AWAFUNGUKIA WAANDAJI WA SHOW YA MAFIKIZOLO
 
Rapper Wakazi amesema waandaji wa show ya Mafikizolo walitakiwa kuwapa nafasi baadhi ya wasanii wa Tanzania kuonesha uwezo wao mbele ya mashabiki wa muziki ambao huwa hawahudhurii sana show zinazoandaliwa na mapromota wa nyumbani.

Amesema walipaswa kuchagua wasanii wanaoweza kwendana na hadhi ya muziki wa Mafikizolo ili watumie fursa hiyo kupata mashabiki wapya na kwamba hilo ni jambo lililomsikitisha. “Sio vibaya wangewapata nafasi wasanii wa nyumbani mbele ya umati kama ule ile wajue kuwa ‘sawa tumekuja kuwaona Mafikizolo lakini nyumbani pia tunao hawa na wenyewe wanaweza wakatubeba’ ili siku zingine ukiwaita wakiwa watu wa nyumbani inawezekana ukawavutia ukapata wateja wa muziki,” amesema Wakazi.
“Hicho ndicho kitu pekee ambacho kidogo kilinisikitisha,”aliongeza.
Hata hivyo Wakazi amesema show ya wasanii hao kutoka Afrika Kusini ilikuwa kali na aliifurahia mwanzo hadi mwisho.

No comments: