Diamond Platnumz amethibitisha kuwa ndiye msanii namba moja kwa sasa nchini Tanzania baada ya usiku wa Jumamosi kunyakua vipengele vyote zote saba alivyokuwa ametajwa kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro, KTMA.
Ommy Dimpoz akiongea kwa niaba ya Diamond Platnumz
Muimbaji huyo aliyekuwa ameambatana na mchumba wake Wema Sepetu amechukua tuzo ya wimbo bora wa mwaka, wimbo bora wa afro pop na video bora ya mwaka kwa wimbo wake ‘My Number On’e pamoja na Muimbaji Bora wa kiume – Kizazi Kipya, Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki na Mtunzi Bora wa Mwaka – Kizazi Kipya.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kulia) akimkabidhi tuzo Diamond, kushoto ni producer wa My Number One, Sheddy Clever
Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu akimkabidhi Fid Q tuzo
Nalo kundi la Weusi limeibuka na tuzo mbili, Wimbo bora wa Hip Hop (Nje ya Box – Nick wa Pili f/ Joh Makini & G-Nako) na Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya.
Weusi wakipokea tuzo
Vanessa Mdee akimbusu Lulu baada ya kukabidhiwa tuzo ya wimbo bora wa R&B
Jose Chameleone akipokea tuzo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki
Wasanii wa Kenya, Amani na Wyre wakimkabidhi tuzo Luiza Mbutu
Isha Ramadhan akipokea tuzo
Wasanii waliotumbuiza kwenye tuzo hizo ni pamoja na Mwana FA, Weusi, Madee, Vanessa Mdee, Meninah, Angel, Makomando, Msami, Twanga Pepeta, Extra Bongo na wengine.
Tazama orodha nzima ya washindi wa tuzo hizo.
No comments:
Post a Comment