Katika tuzo za kili Music Awards zinazofanyika kila mwaka hapa Bongo na kudhaminiwa na kinywaji cha bia ya Kilimanjaro, siku ya jana katika ukumbi wa Mlimani City kulikuwa na shangwe za kufa mtu baada ya mkali kutoka Wasafi Classic ‘Diamond Platnumz’ kunyakuwa tuzo saba zilizoshindanishwa katika vipengele tofauti tofauti, kwa ushujaa huo amevunja record iliyowekwa na msanii Twenty Percent ambaye awali aliwahi kuchukua tuzo tano kwa mpigo sasa kwa Diamond Platnumz jana ameweza kujinyakulia tuzo saba za ‘Wimbo bora wa mwaka’, Mwimbaji bora wa kiume, Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki, Mtunzi bora wa mwaka kizazi kipya, Video bora ya muziki ya mwaka, Wimbo bora wa Afro Pop, Wimbo bora wa kushirikiana.
Huyu ndiyo Mr. Ngololo na tuendelee kutompigia kura katika tuzo ya MTV ili akamilishe ndoto yake.
Huyu ndiyo Mr. Ngololo na tuendelee kutompigia kura katika tuzo ya MTV ili akamilishe ndoto yake.
No comments:
Post a Comment