DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Sunday, May 4, 2014

Historia Concert kufanyika tena karibuni

 
Onesho la Historia la mwanadada Lady Jay Dee, limesogezwa mbele baada ya hali ya hewa ya mvua kuzuia mashabiki waliohudhuria Tranic Plaza, Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam usiku wa jana, kupata burudani kikamilifu zaidi.
 
Katika onesho hili, ili kuwapa ladha wapenzi na mashabiki wa mwanadada Lady jay Dee waliohuduria, wasanii Dabo, Patricia Hillary, Roma Mkatoliki na Baghdad, Professa Jay na pia Machozi Band ikiongozwa na Lady Jay Dee walipanda jukwaani kutumbuiza kidogo.
Baada ya tukio hilo, eNewz tukaongea na Lady Jay Dee ambaye alizungumzia show hii, na kutangaza zawadi ya show nyingine kali ya Historia hivi karibuni katika mazingira ambayo yataruhusu watu kujiachia kufurahia burudani zaidi.

 

No comments: