Staa wa muziki kutoka nchini Kenya, Jaguar kwa jina maarufu, kwa mara nyingine ameonyesha moyo wake upendo kwa kuamua kurudisha shukurani katika gereza la Industrial Area huko Kenya, mahali ambapo alifanya sehemu ya video ya ngoma yake ya 'kioo'.
Jaguar katika ziara yake hii gerezani, mbali na kuwashukuru wafungwa na maafisa gereza kwa ushirikiano, pia aliwabebea zawadi mbalimbali kwaajili ya kuwapatia na wao nafasi ya kufurahi katika kipindi cha sikukuu iliyomalizika ya Pasaka.
Katika ziara hii ya Jaguar ambayo imesukumwa kwa kiasi kikubwa na mafanikio ya Video yake ya Kioo, Jaguar pia ameripotiwa kuahidi kumsaidia kwa nguvu zake zote moja ya mfungwa ambaye ameonyesha kipaji cha kuimba cha aina yake.
No comments:
Post a Comment