DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Sunday, May 4, 2014

Weasel, Pallaso, AK47, Chameleone waingia vitani

Wasanii wa muziki kutoka familia moja huko nchini Uganda, Weasel, Pallaso, AK 47 pamoja na Jose Chameleone, wameendelea kutumia vipaji vyao vikubwa katika kuleta ladha na ushindani katika muziki wa Uganda.
 
Chameleone, Weasel, Pallaso, AK47
Wasanii hawa kwa ujumla wao wameamua kutengeneza makundi mawili na kufanya rekodi ambazo mashabiki wataamua mkali aliyemfunika mwenzake.
Ndugu hawa katika mpango huu wamejigawa ambapo Chameleone amefanya kazi inayokwenda kwa jina Kaleeba akiwa na mdogo wake wa mwisho AK47, huku Weasel pamoja na Pallaso wakitengeneza timu yao na kutoka na rekodi ambayo inakwenda kwa jina Omugongo, rekodi zote hizi zikiwa zimefanya na mtayarishaji mziki mmoja.
Kwa njia ya mtandao, Pallaso ambaye kazi zake nyingi anafanyia huko Marekani, amewataka watu kusikiliza rekodi hizi kali na kuamua ni kundi gani limemfunika mwenzake kutoka familia yao hii ya kimuziki ya wana-Mayanja.

No comments: