Mkali wa michano ambaye anafanya poa hapa Tanzania, Nikki Mbishi a.k.a
Nikki Zohan, ambaye katikati ya mwaka huu anatarajia kuachia albam yake
mpya 'Ufunuo', amesema, hatua yake ya kuachia albam hii ni kipimo cha
ukubwa wa uwezo wake katika rap.
Nikki
Mbishi amesema haya kutokana na imani inayoendelea sasa kwa wasanii na
wadau wa muziki kuwa biashara ya albam za muziki hususan wa Bongoflava
na Hip Hop hailipi, na kuhusiana na hili, hapa anaelezea juu ya
alivyojipanga na albam hii.
Msanii Nikki Mbishi amesema kuwa, wasani wengi hapa nchini wanaogopa
kutoa albam kwasababu ya kutokuamini uzuri wa kazi zao, na pia kutokana
na kutokupenda kazi zao tofauti na yeye ambaye anaajiamini na kuamini
kuwa kazi yake ni nzuri na ni biashara tosha.
No comments:
Post a Comment