Msanii wa muziki wa Genge kutoka nchini Kenya, Nonini pamoja na marafiki
zake wameibuka na njia mpya ya kuchangisha pesa kwaajili ya shughuli za
hisani, na hii ni kupitia mashindano ya wa mpira wa kikapu ambao
huzikutanisha timu mbali.
Mashindano
haya ya mpira wa kikapu yamepatiwa jina (Entertainment With Fun 4
Charity), ambapo kwa mujibu wa Nonini, yatakuwa yakifanyika kila
sikukuu, huku wakiwa wamepanga kukutana tarehe 1 mwezi June tena
kwaajili ya mechi nyingine kali.
Katika mashindano ya kwanza yaliyofanyika, kiasi cha shilingi za
Kenya 120000 zilipatikana, ambapo asilimia 50 ya pesa hizi ilipelekwa
katika kituo cha kulelea watoto cha Filomena kilichopo huko Kayole.
No comments:
Post a Comment