DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, May 2, 2014

Ulokole wamshinda Bamboo

 
Rapa Bamboo ameibuka na jambo jingine jipya ambalo limeanza kuzua maswali juu ya uhalali wa maamuzi yake ya kutangaza kuokoka na kuachana na muziki wa dunia, na hii ni baada ya kuachiwa kwa kazi mpya yenye mrengo wa kidunia.
 
Kazi hii inayokwenda kwa jina Like it or Not, Bamboo ambaye kuokoka kwake kumeenda sambamba na kujibadilisha jina na kujiita Abraham, alitangaza pia mpango wake wa kuwa anafanya ngoma za kueneza ujumbe wa Mungu tu, na kupitia kazi hii mpya anaonekana na wasanii Guru Gang pamoja na Sharama wakiwakilisha yale yale aliyotangaza kuachana nayo.
Mpaka sasa bado hakuna ufafanuzi wowote kutoka kwa Bamboo kuhusiana na hiki kinachoendelea sasa katika kazi zake ikihusianishwa na msimamo wake wa kiimani ambao anaufuata sasa.

No comments: