Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hamisi Ramadhani Baba,maarufu kama
'H.Baba' amefunguka na kusema kuwa wanamuziki wa Bongo fleva sasa
watakata mauno,H Baba alisema hayo alipokuwa akihojiwa na EATV.
H
Baba amesema kuwa wakati anatambulisha muziki wa Bongo Bolingo Fleva
wadau wa mauziki kama hawakuweza kumuelewa na hawakuweza kumpa support
ili muziki huo ufike sehemu nzuri zaidi lakini anashukuru sasa aina ya
muziki aliokuwa akiupigania miaka kadhaa nyuma ndio umeliteka soko la
muziki wa Afrika na unazidi kukua kwa kasi kubwa.
"Wakati nimeanza kufanya Bongo Bolingo Fleva watu hawakunielewa nafanya nini na kuna baadhi ya wasanii wenzangu walikuwa wakinikashifu kuwa H Baba yule ni mkata viuno tu,sasa kwa kuwa muziki huu ndio umeshika chat kwa sasa amini usiamini wasaniii wa Bongo Fleva sasa watakata viuno kama H Baba maana muziki huu unahitaji uwezo wa hali ya juu katika steji ndio maana hata watu ambao wanaufanya wapo vizuri stejini".
H Baba aliongeza kuwa kwa sasa wasanii wakubwa Africa kama P square,Iyanya,Davido na wengine wengi wanafanya muzuki ambao yeye anafanya hivyo kwa kuwa wasanii wengi wamekuwa si wabunifu kubuni vitu vyao hivyo wataanza kufanya huo muziki ila wanapaswa tu kuelewa kuwa muziki huo unahitaji uwezo mkubwa stejini.
Mimi nashukuru sana P Square kuweza kutoa wimbo wao huu wa Test my money ambao umekuwa na vionjo vya bolingo kama ambavyo mimi nafanya Bongo Bolingo fleva maana wimbo huu utasidia aina ya muziki huu kukua na kuenea zaidi na hii itanisaidia mimi maana wao watakuwa wamefanya kazi rahisi kuwaelewesha wadau juu ya aina hii ya muziki ninao fanya hivyo inaweza kunipa nafasi kufanya mambo mazuri zaidi,hivyo hawa wasanii wa Bongo fleva najua watafanya huu muziki lakini wanapaswa kutambua kuwa uhahitaji uwezo wa hali ya juu ukiwa stejini,hivyo wajipange kukata mauno tu.
Akizungumzia Wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Tubebane,H Baba amedai kuwa wimbo huo hakuutambulisha bali umevuja baada ya gari yake ndogo kuvunjwa kioo na kuibwa kwa baadhi ya vitu ikiwemo Flash ambayo ilikuwa na wimbo huo ndipo ilivuja,amedia kuwa haukuwa wakati wake kuachia wimbo huo kwa sasa kwa kuwa bado alikuwa akiendelea kujiandaa ili kuja kutambulisha wimbo huo siku za usoni.

No comments:
Post a Comment