DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, March 27, 2014

SHAA AHOJI KWANINI HAJAWA NOMINATED KATIKA KTMA 2014


 SHAA AHOJI KWANINI HAJAWA NOMINATED KATIKA KTMA 2014

Baada ya majina ya waliochaguliwa kuingia katika nominations za tuzo za Kili Tanzania Music Awards 2014 kutolewa wiki hii, wasanii na wadau mbalimbali wamepokea kila mmoja kwa hisia tofauti. Mwimbaji wa ‘Sugua Gaga’ Shaa ambaye hakufanikiwa kuingia amezungumzia jinsi alivyopokea nominations hizo.

“Kwa jinsi ninavyosikia ni kwamba kura za wananchi hazikuzingatiwa,” Alisema Shaa kupitia Clouds E ya Clouds TV. “kwa asilimia kubwa kura za wananchi wale watu waliowapendekeza hazijazingatiwa, sijui kwanini na ningependa kujua kwanini kwasababu nilivyosikia vitetesi vya hapa na pale wimbo wa Sugua Gaga ulikuwepo, aah kwahiyo nataka kufahamu kwanini wananchi mmewahusisha wasuggest kwamba Shaa awepo na wimbo huu uwepo halafu kwanini basi mwisho wa siku hamjazingatia hilo.”
Shaa ameongeza kuwa hakuna kitu alichopoteza wala kuongeza kwa kutopendekezwa na haijamuuma kutokuwa nominated katika Tuzo lakini kinachomuuma ni kuwahusisha wananchi waliompigia kura na bado asichaguliwe.
“Kuhusu msimamo wangu mimi mwenyewe kutokuwa nominated…mwisho wa siku mi naangaliaga nina gain kitu gani kwenye nominations aah nipo kwenye game huu ni mwaka wangu wa tano nimewahi kuwa nominated kwenye Kili Awards mara tatu…kwangu mimi nikiangalia sijapoteza kitu chochote na wala sija gain kitu chochote. Kwahiyo kwangu mimi kusema ukweli haijaniuma…ukweli kabisa haijaniuma kilichoniuma ni hiyo tu kwamba kwanini mwananchi, tena hata mimi nikachukua muda walivyokuwa wanasema aah mbona nyie watu wenyewe hamuhamasishi watu, nikachukua muda wa kumlipa mtu atengeneze flier ili nihamasishe mtu apige kura na huyo mtu akaiona hiyo flier akatumia vocha. Kwahiyo kwangu mimi ni hicho tu kilichoniuma kwamba kama system ilikuwa haihitajiki kwanini ilikuwepo pale.” Alimaliza Shaa

No comments: