wanamuziki kutoka “Malaika music band” Christian Bella ameamua kujitupa
kufanya muzuki ambao utakuwa tofauti kidogo na muziki ambao amekuwa
akifanya kwa miaka kadhaa,akiwa na lengo la kuleta ladha tofauti katika
muziki wake na kuongeza mashabiki
Christian
Bella alisema kuwa kwa sasa anaanza kutambulisha wimbo wake mpya ambao
amemshirikisha msanii Ommy Dimpoz,wimbo ambao umefanywa katika studio za
Combination Sound chini ya produza Man Walter.
Ni kweli nimefanya aina tofauti ya muziki kwa sasa natambulisha Bongo
fleva niliyofanya na rafiki yangu Ommy Dimpoz,wimbo unaitwa 'Nani kama
mama' na nitautambulisha mwezi April mwanzoni,nitatoa Audio na Video
kwa pamoja ili mashabiki waweze kupata burudani na kupata kumsikia na
kumuona Bella akifanya Bongo Fleva"
Christian Bella aliongeza kuwa huo ni mpango wake kwa sasa
kuchanganya ladha katika muziki wake hivyo mashabiki wakae teyari tu
kwani kuna wimbo wa RNB utafuata baada ya Nani kama mama,wimbo ambao
anafikiri kufanya na mwanamuziki wa Rnb wa hapa nyumbani huku
akichanganya na msanii mwingine wa Hip Hop.
Christian Bella alishawahi kuwa Prezidaa wa Bendi ya Akudo Impact
'Vijana wa Masauti' kwa miaka kadhaa kabla ya kuachana na Bendi hiyo na
kuanzisha Bendi nyingine inayofahamika kama 'Malaika music band”.
No comments:
Post a Comment