Bila shaka kama wewe ni shabiki wa Alikiba hukujiuliza mara mbili
kuupakua wimbo wa ‘Rosa’ ambao umesambaa wiki hii katika mitandao kama
comeback ya star huyo aliyekaa kimya kwa muda mrefu.
Lakini cha kushangaza ni kuwa Alikiba mwenyewe hautambui wimbo huo sababu hauko kwenye orodha ya nyimbo alizowahi kurekodi na wala hafahamu mtu aliyeuimba.
Lakini cha kushangaza ni kuwa Alikiba mwenyewe hautambui wimbo huo sababu hauko kwenye orodha ya nyimbo alizowahi kurekodi na wala hafahamu mtu aliyeuimba.
Alikiba amesema amepigiwa simu na vituo vya redio vikimuuliza kuhusu
wimbo wake mpya walioupata uitwao ‘Rosa’ lakini hana taarifa nao.
“Nyimbo zipo lakini sija release nyimbo…sijatoa nyimbo so far na
sijui nani ameimba na sijawahi hata kuisikia” Alisema Alikiba
alipozungumza na mtangazaji Renatus Kiluvya kupitia New Chapter ya Radio
Free Africa.
“Sijawahi kuisikia na sitaki kutoa comment yoyote kwasababu
navyojijua mimi first of all najikubali sana, la pili watu wananiambia
niko unique afu surprise watu wananiambia nimetoa nyimbo sijui tumesikia
nyimbo inaitwa Rosa yaani hiyo sijaelewa bado.” Alisema hit maker wa
Cinderella.
Aliongeza kuwa kuna uwezekano kuwa kuna watu wamefanya makusudi
kufake wimbo huo uonekane ni wake kutokana na ukimya wake, au wamefanya
sayansi sauti isikike kama yake, au huyo aliyeimba ni role model wake
ndio sababu kaamua kufanya hivyo.
“Wameona nimekaa kimya sana wakaona ngoja watoe nyimbo na wakatumia
jina la Alikiba, it doesn’t make sense kama unatoa nyimbo unategemea
kutoka kwa jina la mtu flani, I think ni trick moja ambayo imefanywa
sielewi na nani lakini I don’t know if in a good way or bad way.”
Pia Ali K alizungumzia ujio wake mpya,
“Ujio wangu uko very soon, sasa hivi wakae tayari fans wangu na kilichonifanya nikae kimya kingi watajua ni kitu gani na watani understand kabisa maana ya kukaa kimya.”
“Ujio wangu uko very soon, sasa hivi wakae tayari fans wangu na kilichonifanya nikae kimya kingi watajua ni kitu gani na watani understand kabisa maana ya kukaa kimya.”
No comments:
Post a Comment