Msanii Diamond Platnumz, ameendelea kuchana mawimbi katika anga la
Afrika ambapo amefanikiwa kuingia katika orodha ya wasanii 20 Bora ambao
wanafanya vizuri Afrika, watakaoingia katika kinyanganyiro cha kuwania
tuzo za Kora.
Diamond
katika orodha hii, anatokea sambamba na majina ya wasanii wakubwa
Afrika, kama vile Oliver Mtukudzi, Fally Ipupa, Mafikizolo pamoja na
wakali wengine wa muziki barani Afrika.
Kutokea kwa Diamond katika orodha hii, ni nafasi nyingine kubwa ya
kuipeperusha bendera ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, katika
jukwaa la kimataifa.
Kwa sasa mchakato unaendelea kupitia ukurasa wa facebook wa Tuzo
hizi, ambapo maoni mbalimbali ya mashabiki yanakushanywa kuhusiana na
wasanii gani wanaokubalika zaidi, tayari kwa kuwapambaniza katika tuzo
hizo kubwa.
No comments:
Post a Comment