Msanii Diamond Platinumz, amesema kuwa, kwa sasa baada ya mafanikio
makuwa ya remix ya ngoma yake ya My Number One, picha linaendelea ambapo
atawazawadia mashabiki wake kolabo nyingine kubwa ya kimataifa hivi
karibuni.
Diamond
amesema kuwa, harakati anazofanya sasa ni kufanya Tanzania na muziki
wake ufike mbali zaidi, ambapo amefichua kuwa, amekuwa akipokea maombi
mengi kutoka kwa wasanii wa nje kwa ajili ya kufanya kolabo nae, na hapa
anaeleza juu ya mchongo huu, vile vile kolabo nyingine za kimataifa
ambazo zitatoka baada ya My Number one Remix.
Msanii huyu amesema pia, baada ya kuusoma vizuri muziki barani
Afrika, amegundua kuwa kuna soko kubwa la muziki wa Afrika Magharibi, na
pia kuna soko la muziki wa Afrika kwa ujumla, na sasa atakua akitoa
ngoma zake kwa kufuata ramani ya soko hili.
Diamond pia amewakata mashabiki wake kufahamu kuwa, hivi karibuni
kuna kazi kubwa ambazo amefanya na Iyanya pamoja na D'banj ambao ni
wasanii wakuba Nigeria, kazi ambazo zinatarajia kutikisa vilivyo pindi
zitakapotoka.
No comments:
Post a Comment