sanii wa muziki, Linex Sunday Mjeda, baada ya kusumbua sana katika chati
mbalimbali za muziki na ngoma yake ya Kimugina, kwa sasa ameamua
kuunganisha nguvu na Jambo Squad kutoka Arusha kupitia kolabo ambayo
imesukwa chini ya studio za Noize Makers.
Linex
ambaye katika rekodi za muziki wake, hii inakuwa ni kazi ya kwanza
kabisa kufanya na wasanii kutoka Arusha ikiwa pia ni aina tofauti kabisa
ya muziki ambayo amewahi kufanya.
Kazi hii itatoka hivi karibuni ikiwa na matarajio makubwa ya
kuunganisha mashabiki wa muziki kutoka pande mbili, wale wanaokubali
zaidi kazi za Jambo Squad kutoka Kaskazini mwa Tanzania, na wale wa
Linex ambaye muziki wake unawavutia watu wa rika mbalimbali ndani na nje
ya mipaka ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment