Kigwema ambaye kwa sasa amekuwa kimya katika muziki amedai ameamua
kuanza na project ya Narudi nyumbani ambayo itakuwa maalumu kwa watu wa
kusini kabla ya kuachia kazi mpya aliyofanya na Stara Thomas.
"Nilipanga kuachia wimbo wangu mwezi wa tatu lakini kuna wadau wa
muziki na wasanii wakongwe walinipa maoni yao na kunishauri hiyo kazi
niifanye kwa P Funk nikasikiliza maoni yao na nimeanza kuyafanyia kazi
lakini nimeona nisiwe kimya ndio maana nimekuja na Project ya Narudi
nyumbani ambayo hii project imelenga watu wangu wa kusini kwa kuwa muda
mwingi niko kule hivyo nisikae kimya muda wote mkapa hapo kazi yangu
mpya itakapotoka"
Akizungumzia project narudi nyumbani amedai kuwa kuanzia Jumamosi
wataanza kutengeneza Video ya narudi nyumbani na wataanzia Somanga mpaka
Mtwara na hii yote ni kushow upendo wa watu wake wa kusini ambao muda
mwingi wamekuwa wakimpa hamasa ya kufanya kazi nzuri zaidi na kumfanya
afurahie kuishi kusini.
Kigwema alishawahi kutamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo Sintomshau,Kwenye magazeti na zingine nyingi.
No comments:
Post a Comment