BAADA ya Baraza la
Sanaa Taifa (BASATA), kuondoa nyimbo ya msanii wa muziki wa kizazi kipya
Madee, nyimbo inayojulikana kwa jina la Tema mate Tuwachape, mapya yaibuka ambapo msanii huyo adai kuwa Baraza hilo limechelewa kufanya maamuzi.
Msanii huyo amedai kuwa baraza hilo limechelewa kufanya maamuzi
hayo ya kuuondoa wimbo huo katika kinyg’aganyiro hicho ikiwa nyimbo hiyo
imeshapigwa kwa muda wa mwka mzima sasa.
Madee ametoa ushauri kwa baraza hilo kuwa ni vyema wakaweka chombo
maalumu cha kuhakiki nyimbo zao kabla hazijapelekwa kwa mashabiki hali
hiyo itasaidia kurekebisha makosa.
Aliongezea kuwa kuondoa wimbo huo katika kinyanga’nyiro hicho
hawajatenda haki kwani nyimbo yake imeshikiria chati kwa muda mrefu
kwenye redio mbalimbali, hivyo ni sawa na kuwadhurumu mashabiki wake.
Alienda mbali zaidi ambapo anadai kuwa kauli hiyo ya kuondolewa
haijamshtua sana kwani hajawahi kupokea tuzo yoyote tangu ameanza kazi
ya muzi.
Nyimbo ya Madee, ni miongoni mwa nyimbo zilizoenguliwa katika mchakato wa kinya’nganyiro cha tuzo hizo.
No comments:
Post a Comment