DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Sunday, March 23, 2014

Mambo 10 usiyoyajua kumhusu Wyre kutoka Kenya


 

Ameshinda tuzo nyingi sana kutokana na aina yake ya uimbaji, ambao ni Reggae na Dancehall. Pia umaarufu wake uliongezeka zaidi pale alipomshirikisha katika nyimbo yake mwanadada Alaine katika wimbo wake wa “Nakupenda Pia” Kama bado hujamjua namzungumzia Wyre kutoka kenya.
 
Pamoja na kua ni maarufu sana lakini ni mambo machache sana yanajulikana kuhusu maisha yake ukiachana na mziki. Akifanya mahojiano na Tovuti ya Niaje ya Kenya, Wyre aliamua kutaja mambo kumi hatuyajui kuhusu yeye
  1. Gari yake ya kwanza kumiliki ilikua Subaru impreza
  2. Anapendelea zaidi magari yanayotengenezwa na kampuni ya BMW
  3. Hatumii madawa au kilevi cha aina yeyote ile
  4. Mchumba wake wa kwanza alimpata akiwa darasa la 8.
  5. Mwanamke wa ndoto zake ni mke wake aliye nae sasa.
  6. Amesomea mass communication
  7. Mara yake ya kwanza kuperform stejini ni alipokua High School ambapo alifanya akapela akiwa na rafiki zake.
  8. Anasema bado anahitaji kujulikana zaidi.
  9. Kwenye upande wa mavazi anapenda nguo za Sean John
  10. Siku ambayo hatasahau ni siku aliyoshinda tuzo ya msanii chipukizi katika tuzo za International Reggea Awards.

No comments: