DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Sunday, March 23, 2014

MAPROFESSOR WA MUZIKI TANZANIA.


 

Katika historia ya muziki Tanzania kuna watu wa-3 tu waliopata kuitwa ma-professor. Mmoja kwenye muziki wa dansi (BONGO DANSI), mmoja Taarab na mwingine bongo flava.

Kwenye BONGO FLAVA kuna Professa Jay wa Mitulinga, Joseph Haule. Huyu jamaa ameanza kujulikana zaidi tokea enzi za Hard Blasters Crew (HBC) akiwa na Fanani na Willy. Watu wanakumbuka wimbo wa Chemsha Bongo” na “Mamsapu”.Kwenye TAARAB kuna mtu alikuwa anaitwa Professor Mohamed Mrisho. Huyu alipata kutunga wimbo wa
“Nyama ya Bata” alipokuwa na TOT Plus miaka ya mwanzoni mwa 1990. Wimbo huu ulikuwa katika album ya “TX MPENZI”, albamu ambayo pia ilikuwa na wimbo makini wa “Zumbukuku” uliotungwa na Ally Star.
Kwenye MUZIKI WA DANSI kulikuwa na Professor Omar Shaaban. Huyu alikuwa ni bingwa wa kupiga rhythm guitar Africa Mashariki na kati miaka ya 70 na 80. Huyu ni mmoja wa waanzilishi wa kundi la Simba Wanyika. Baadaye alikuwa ndio kiongozi wa maasi ya mwaka 1978 yaliyosababisha kundi kugawanyika na kuzaliwa Les Wanyika.

Kwenye picha huyu ndiye Professor Omar Shaaban ambaye ni mtunzi wa wimbo wa “Sina Makosa”, wimbo wa pili kwa umaarufu kuliko nyimbo zote zilizopata kutokea katika historia ya Afrika Mashariki.
Katika hawa maprofessor watatu, wawili wameshatangulia mbele za haki. Mmoja alizikwa Tanga, Tanzania. Mwingine alizikwa Nairobi, Kenya makaburi ya Langata.


No comments: