anii Young Killer ambaye amerudi kwa kasi katika chati za muziki na
ngoma yake mpya ambayo inakwenda kwa jina “My Power” ambayo
amemshirikisha Damiani Soul, amesema tangu afahamike na wengi kupitia
muziki, amepoteza idadi kubwa ya marafiki.
Tofauti na wengi walivyotegemea, Young Killer amesema kuwa, Muziki
umempunguzia marafiki, lakini pia rapa huyu akakiri kuwa muziki huu huu
umemkutanisha na kumpatia nafasi ya kufahamiana na watu wengi.
Young Killer pia amezungumzia ukali wa ngoma zake ambapo amesema
kuwa, yeye hutumia muda mrefu sana katika kuandika mashairi ya muziki
wake, kitu ambacho kinafanya mashairi yake kukubalika kwa kiasi kikubwa
kila kukicha na idadi kubwa ya watu.
No comments:
Post a Comment